Home Habari Kuu Idara ya magereza yaonya dhidi ya unyanyapaa kwa wafungwa waliotoka jela

Idara ya magereza yaonya dhidi ya unyanyapaa kwa wafungwa waliotoka jela

0
Naibu Kamishna wa Magereza nchini Florence Omondi
Naibu Kamishna wa Magereza nchini Florence Omondi

Idara ya magereza nchini sasa inawataka Wakenya sawia na jamii kwa jumla kukomesha unyanyapaa dhidi ya wafungwa waliorudi kwa jamii kutoka gerezani.

Kulingana na Naibu Kamishna wa Magereza nchini Florence Omondi, hali hiyo imechangia wengi wa watu waliotumikia kifungo kufanya makosa zaidi hata baada ya kutoka jela kutokana na unyanyapaa.

Amesisitiza haja ya wafungwa waliomaliza kifungo na kurudi nyumbani kupokelewa vyema na jamii badala ya kutengwa.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Askofu wa jimbo la Mombasa Alphonce Mwaro ambaye amesistiza haja ya jamii kuwakubali wafungwa pindi wanapotangamana na familia zao baada ya kifungo.

Dickson Wekesa
+ posts