Home Kimataifa Idadi ya waliofariki katika tetemeko la ardhi Japani yafika 62

Idadi ya waliofariki katika tetemeko la ardhi Japani yafika 62

0

Onyo la kutokea tsunami limeondolewa nchini Japani baada ya tetemeko kubwa la ardhi, lakini idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 62, huku nyumba zikiharibiwa.

Waziri Mkuu wa Japani, Fumio Kishida amesema idadi ya waliojeruhiwa na kiwango cha uharibifu ni kikubwa.

Takribani watu elfu moja kutoka timu za uokoaji wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu wanaoaminika kukwama chini ya vifusi vya nyumba.

Jeshi la Japani linatoa vifaa vya msaada ikiwa ni pamoja na kusambaza maji, chakula na mablanketi.

Onyo la tsunami kando ya Bahari ya Japani limeondolewa, kumaanisha hakuna hatari tena ya tsunami.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema yuko tayari kutoa msaada unaohitajika kwa Japani.

BBC
+ posts