Home Kimataifa Idadi ya waliofariki katika shambulizi la Moscow yaongezeka hadi 113

Idadi ya waliofariki katika shambulizi la Moscow yaongezeka hadi 113

Serikali ya urusi imetangaza kuwa watu 11 wamekamatwa, wakiwemo washukiwa wanne wa uvamizi huo.

0
Mashambulizi yatekelezwa Jijini Moscow, Urusi.

Idadi ya waliofariki kutokana na shambulizi la Ijumaa jioni lililotokea katika ukumbi wa jiji la Crocus viungani mwa mji wa Moscow, imeongezeka na kufikia watu 133, huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.

Wanachama wa kundi la Islamic State, ambao walikiri kuhusika na shambulizi hilo, waliwafyatulia risasi walinzi kwenye lango la jumba hilo la kitamaduni, kisha wakawashambulia watu waliokuwa wakitazama tamasha hiyo.

Kulingana na uchunguzi wa hivi punde uliofichuliwa leo Jumamosi, washambuliaji hao waliingia kwenye tamasha hiyo na kisha kuwasha moto jengo hilo.

Serikali ya urusi imetangaza kuwa watu 11 wamekamatwa, wakiwemo washukiwa wanne wa uvamizi huo.

Rais Vladimir Putin alisema leo kwamba watu hao wanne waliojihami wamekamatwa, ambapo aliahidi kukabiliana vilivyo na waliohusika na shambulizi hilo.