Home Habari Kuu Idadi ya waliofariki katika mkasa wa moto Embakasi yaongezeka

Idadi ya waliofariki katika mkasa wa moto Embakasi yaongezeka

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura, alidokeza kuwa idadi ya majeruhi imeongezeka kutoka 222 hadi  280.

0

Idadi ya waliofariki katika mkasa wa moto uliotokea Embakasi Jiji Nairobi, imeongezeka hadi watu watatu.

Akithibitisha hayo alipozuru eneo la mkasa Ijumaa asubuhi, msemaji wa serikali Isaac Mwaura, alidokeza kuwa idadi ya majeruhi pia imeongezeka kutoka 222 hadi  280.

“Awali tulikuwa na vifo viwili lakini sasa watu  watatu wamefariki. Serikali inatuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu,” alisema Mwaura.

Kati ya majeruhi hao 280, 43 wamepelekwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu zaidi.

Wengine 157 wanapokea matibabu katika hospitali ya Mama Lucy huku 18 wakiwa wanahudumiwa kwenye hospitali ya Komarock Modern.

Kulingana na Mwaura waathiriwa 17 wengine wamelazwa katika hospitali ya Mafunzo ya Chuo cha Kenyatta, 21 katika hospitali ya Garrison, wanane katika hospitali ya Metropolitan na wawili wanatibiwa katika hospitali ya Radiant.

Mgonjwa mmoja yuko katika hospitali ya Pendo, watatu katika AAR na wanne Hospitali ya Nairobi.

Mkasa huo wa moto ulitokea usiku wa kuamkia Ijumaa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Alphas Arap Lagat
+ posts