Home Kaunti Idadi ya maafa katika ajali ya Londiani yafika 52

Idadi ya maafa katika ajali ya Londiani yafika 52

0

Takriban watu 52 wamethibitishwa kufariki, baada ya lori kugonga magari kadhaa eneo la Londiani katika barabara kuu ya Kericho-Nakuru Ijumaa jioni.

Kulingana na waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen, watu wengine 35 wanapokea matibabu katika hospitali mbali mbali.

Ajali hiyo ilitokea Ijumaa saa kumi na mbili na nusu jioni, baada ya trela kupoteza mwelekeo na kugonga magari kadhaa, watu waliokuwa wakitembea kwa miguu, wanabiashara na magari ya uchukuzi wa umma zilizokuwa zimeegeshwa kando ya barabara.

Lori hilo lilikuwa likielekea Kericho, kabla ya kupoteza mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, dereva wa lori hilo alikuwa akiepuka kugonga basi moja lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara baada ya kukumbwa na hitilafu.

Seneta wa kaunti ya Kericho Senator Aaron Cheruyiot, ambaye alizuru eneo la ajali alisema serikali ya kitaifa inapaswa kufungua rasmi hospitali ya kaunti ndogo ya Lodoiani, huku akitaja ukosefu wa vituo vya afya katika eneo hilo.

Alisema hospitali nyingi katika kaunti ya Kericho zilishuhudia idadi kubwa ya majeruhi, huku waathiriwa wakipelekewa katika hospitali mbali mbali.

Gavana wa Kericho Dkt. Erick Mutai, amesema serikali ya kaunti hiyo italipa bili za hospitalini na zile za upasuaji wa maiti pamoja na kuzisaidia familia zilizoathirika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here