Home Habari Kuu Utapeli? Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Mudavadi anaswa

Utapeli? Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Mudavadi anaswa

0
kra

Mkurugenzi wa Mawasiliano katika afisi ya Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi Salim Swaleh alikamatwa na maafisa wa ujasusi  Jumamosi jioni kwa tuhuma za kuhusika katika sakata  ya ulaghai na utapeli.

Swaleh anadaiwa kuunda vitambulisho bandia vya kazi na funguo za milango kwa raia wa kigeni waliokuwa wakitekeleza shughuli zao haramu katika afisi ya Mudaadii iliyopo eneo la Railways jijini Nairobi.

kra

Kulingana na taarifa kutoka kwa Katibu wa Mawasiliano ya Kimikakati katika afisi hiyo Peter Warutere, uchunguzi ungali unaendelea ili kuwanasa washukiwa zaidi.

Swaleh pia anadaiwa kujaribu kuwahonga maafisa wa upelelezi waliomnasa ili kuzima sakata hiyo.

Kabla ya kuteuliwa Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ofisi ya Mudavadi, Swaleh alifanya kazi kama mtangazaji katika kituo kimoja cha runinga humu nchini.

Haijabainika ni lini atafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayomkabili, ingawa upo uwezekeno mkubwa wa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu kwa mujibu wa katiba.

Sheria haikubali mshukiwa kuzuiliwa kwa zaidi ya saa 24 kabla ya kufikishwa mahakamani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here