Home Michezo Hussein Mohammed apongeza uzinduzi wa Talanta Plaza

Hussein Mohammed apongeza uzinduzi wa Talanta Plaza

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika la Extreme Sports Hussein Mohammed, amempongeza Rais William Ruto na Waziri wa Michezo Ababu Namwamba kwa uzinduzi wa jengo jipya la Talanta Plaza

0

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika la Extreme Sports Hussein Mohammed, amempongeza Rais William Ruto na Waziri wa Michezo Ababu Namwamba kwa uzinduzi wa jengo jipya la Talanta Plaza eneo la Upper Hill kaunti ya Nairobi.

Hussein amesifia pia hatua ya kutenga chumba maalum cha kuweka picha na vinyagovya mashujaa wa michezo nchini katika jumba hilo, kama njia ya kuwatambua wanaspoti waliotia fora na kuiletea nchi sifa katika mashindano ya kimataifa.

Rais William Ruto akifungua jengo la Talanta Plaza

Bw. Hussein ambaye pia amekuwa mkereketwa wa soka nchini amesema hatua ya kuweka picha hizo za wachezaji katika jengo hilo inawatia morali wanaspoti wengine na kuwatia hamasa kufanya vyema viwanjani.

Afisa huyo mkuu wa Extreme Sports alipata fursa ya kutangamana na wanamichezo kadhaa akiwemo bingwa mara tatu wa dunia na bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon,mchezaji wa zamani wa klabu ya Inter Milan na timu ya taifa Harambee Stars Mc Donald Mariga na mshindi wa kwanza wa dunia kutoka Kenya katikambio za Marathon Catherine Ndereba miongoni mwa wengine.

Website | + posts