Home Kimataifa Hunter Biden afunguliwa mashtaka ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria

Hunter Biden afunguliwa mashtaka ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria

Wakili wa Hunter, Abbe Lowell amekashifu Weiss kwamba ameshinikizwa kisiasa na upande wa Republican katika kumfungulia mashitaka.

0
Hunter Biden, mwanawe Rais wa Marekani Joe Biden.

Hunter Biden, mwana wa kiume wa Rais wa Marekani Joe Biden jana Alhamisi alifunguliwa mashtaka, akituhumiwa kununua bunduki katika muda aliokiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine, wakati akidanganya kuwa hakuwa akitumia ili aweze kuuziwa silaha hiyo.

Mashtaka hayo dhidi ya Hunter mwenye umri wa miaka 53 mara moja yamezua mjadala mpya kwenye kampeni za urais nchini Marekani mwakani.

Baba yake Joe Biden anapanga kuwania tena urais wakati mpinzani wake mkuu wa chama cha Republican Donald Trump akikabiliwa na mashtaka manne ya jinai, yenye jumla ya kesi 91 za kusikilizwa.

Mashtaka dhidi ya Hunter Biden hayakuwa yakitarajiwa, kwa kuwa mwongoza mashtaka maalum David Weiss siku chache zilizopita alisema kwamba yangewasilishwa mwishoni mwa mwezi.

Wakili wa Hunter, Abbe Lowell, amekashifu Weiss kwamba ameshinikizwa kisiasa na upande wa Republican kumfungulia mashtaka.