Home Kaunti Huduma zaboreshwa na ujio wa mtambo wa kutengeneza Oxygen Transmara

Huduma zaboreshwa na ujio wa mtambo wa kutengeneza Oxygen Transmara

0
kra

Huduma katika hospitali ya kaunti ndogo ya Trans Mara Level 4 zimepigwa jeki kufuatia kuwekwa kwa mtambo wa kutengeneza hewa muhimu ya Oxygen hospitalini humo.

Msimamizi wa hospitali hiyo Daktari Samwel Misoi anasema mtambo huo una uwezo wa kuzalisha lita 600 za hewa hiyo kwa muda wa saa 24, na sasa hawalazimiki kuomba hewa hiyo kutoka Kisii na maeneo mengine.

kra

Misoi alisema pia kwamba wamefanya juhudi na kuhakikisha kwamba kila kitanda hospitalini humo kinaweza kuunganishwa na hewa hiyo mara moja kulingana na mahijati ya wagonjwa.

Kando na hayo, hospitali hiyo sasa inatoa huduma kwa saa 24 kila siku kufuatia kuwepo kwa vifaa muhimu kama chumba cha upasuaji, kitengo cha kuhudumia majeruhi, maabara yenye vifaa, mashine za radiolojia na duka la dawa.

Chumba cha kuhifadhia maiti pia kipo kwenye hospitali hiyo na kina uwezo wa kuhifadhi hadi miili 36 kwa wakati mmoja.

Misoi sasa anatoa wito kwa wakazi waeneo la Trans Mara na maene ya karibu watumie hospitali hiyo ya serikali kikamilifu kwa manufaa yao badala ya kusafiri mbali ktafuta huduma.

Kina mama wajawazito nao wanahimizwa kujifungulia huko na wala sio nyumbani ili waweze kupokea huduma kutoka kwa wahudumu wa afya waliohitimu.

Misoi alimpongeza gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu kwa kuboresha vituo vya afya kote katika kaunti hiyo tangu alipoingia mamlakani.

Muuguzi mkuu katika hospitali hiyo Evelyn Siparoh, alirejelea matamshi ya Misoi akisema mtambo wa Oxygen umeimarisha kwa kiasi kikubwa hadhi ya hospitali ya Trans Mara Level 4.

Website | + posts
Stanley Mbugua
+ posts