Home Kimataifa Huduma za NTSA kutatizika kati ya Disemba 29 na Januari 1

Huduma za NTSA kutatizika kati ya Disemba 29 na Januari 1

0

Huduma za Halmashauri ya Uchukuzi na Usalama Barabarani nchini, NTSA zitatatizika baina ya Ijumaa, Disemba 29 na Jumatatu, Januari mosi mwaka 2024, kutokana na uhamishaji wa huduma hadi mtandao wa e-Citizen.

Hali hiyo itawaathiri wateja wote wanaohitaji huduma za NTSA katika afisa zake na pia kupitia mtandaoni ikiwemo maombi ya leseni.

Mashirika yote ya serikali kote nchini yalipewa makataa ya hadi mwezi ujao kuhamisha huduma zao hadi katika mtandao wa e-Citizen ili kuboresha utoaji huduma.

Website | + posts