Home Habari Kuu Hospitali ya Mama Margaret Uhuru yafunguliwa rasmi

Hospitali ya Mama Margaret Uhuru yafunguliwa rasmi

0
Hospitali ya Mama Margaret Uhuru katika mtaa wa Korogocho.
kra

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja, amefungua rasmi hospitali ya Mama Margaret Uhuru iliyoko katika mtaa wa Korogocho.

Hospitali hiyo iliyo na vitanda 548 vya wagonjwa, hivi majuzi ilihamishwa kutoka kwa usimamizi wa serikali kuu hadi ile ya Kaunti ya Nairobi, sasa ni mojawapo ya vituo vikuu vya afya katika Kaunti ya Nairobi.

kra

Akiongea na wakazi wakati wa uzinduzi huo, Sakaja alisema hospitali hiyo itawahudumia wakazi wa Korogocho na Kaunti nzima kwa jumla.

Aidha, aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo uwasilishaji wa huduma bora ya afya huku akipuuzilia mbali wasiwasi kuwa uhamisho huo huenda ukaathiri utendakazi wa hospitali hiyo.

“Kufunguliwa rasmi kwa hospitali hii iliyo na vitanda 548, kunahitimisha safari iliyoanza mwaka 1988,” alisema gavana Sakaja alipofungua rasmi hospitali hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here