Home Habari Kuu Hospitali ya KUTRRH yawaajiri madaktari wa kigeni

Hospitali ya KUTRRH yawaajiri madaktari wa kigeni

Mwenyekiti wa Bodi ya wasimamizi wa hospitali hiyo Prof. Olive Mugenda, alisema madaktari watatu, mmoja raia wa Ethiopia,Tanzania na  Malawi, wameajiri wa na hospitali hiyo.

0
Hospitali ya rufaa na mafunzo ya chuo kikuu cha Kenyatta.

Huku mgomo wa madaktari ukiingia wiki ya nne, Hospitali ya Mafunzo,Rufaa na Utafiti ya chuo kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), imewaajiri wataalam watano wa matibabu ya saratani kutoka nchi jirani.

Mwenyekiti wa Bodi ya wasimamizi wa hospitali hiyo Prof. Olive Mugenda, alisema madaktari watatu, mmoja raia wa Ethiopia,Tanzania na  Malawi, wameajiri wa na hospitali hiyo.

Akizungumza na wanahabari katika hospitali hiyo, Prof. Mugenda alisema madaktari hao watasaidia pakubwa kufufua kitengo cha kuwashughulikia wagonjwa wa Saratani, ambacho huduma zake zilikuwa zimedumazwa na mgomo unaoendelea wa madaktari.

Kulingana na Mugenda, wagonjwa watano amabo walikuwa wakipokea matibabu ya saratani lakini wakalazimika kwenda nyumbani kutokana na mgomo huo, wameshauriwa kurejea hospitalini.

Alisema hatua ya kuwaajiri madaktari hao imeidhinishwa na serikali, na watasalia katika hospitali hiyo hata baada ya mgomo wa madaktari kukamilika.

“Hospitali hii hupokea idadi kubwa sana ya wagonjwa wa saratani, na huduma za madaktari hawa zitahitajika pakubwa katika kituo hiki cha afya,” alisema Prof. Mugenda.

Aidha, Mugenda alisema hospitali hiyo imewafuta kazi baadhi ya madaktari wake wanaoshiriki mgomo, kwa madai ya kushiriki mgomo uliopigwa marufuku.

“Katika hospitali hii, madaktari 132 wanashiriki mgomo, huku madaktari 82 wakiwa kazini,” aliongeza Mugenda.

Website | + posts