Hoja ya kumbandua madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua, huenda ikawasilishwa bungeni Jumanne juma lijalo, iwapo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula ataidhinisha.
Kulingana na naibu kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Owen Baya, aliyewasilisha hoja hiyo amekusanya takriban sahihi 260, kiwango ambacho kimezidi sahihi 177 zinazohitajika kikatiba.
Naye Kinara wa bunge la Kitaifa, Silvanus Osoro, amesema wabunge wameazimia kujadili hoja ya kumtimua Gachagua itakayowasilishwa na wakili bungeni.
Mbunge wa Teso Kusini Mary Emase ametoa wito kwa wabunge wote katika miungano ya kisiasa kuunga mkono hoja ya kumng’atua Gachagua itakapowasilishwa.
Gachagua amepuuzilia mbali madai ya wale wanaoshabikia kuondolewa kwake akisema ametimiza wajibu wake kwa mujibu wa katiba.