Home Michezo Historia ya mashindano ya Safari Rally

Historia ya mashindano ya Safari Rally

Sebastian Ogier aliibuka mshindi wa WRC Safari Rally mwaka 2021 akiendesha gari la Toyota Gazoo naye Kalle Rovanpera akatwaa ushindi mwaka 2022  pia kutoka kampuni ya magari ya Toyota Gazoo. 

0

Mashindano ya mbio za magari ya WRC Safari Rally yalianzishwa mwaka 1953, yakifahamika kama East African Coronation Rally yakiwa mashindano ya  kuadhimisha kuapishwa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza aliyekuwa likizoni nchini Kenya mwaka 1952.

Lakini chimbuko la mashindano ya Safari Rally lilitokana na Eric Cecil mpwa wake Neil Vincent na rafikiye Eric Tromp, walipokuwa wakibugia mvinyo kwenye baa moja mjini Limuru mwaka 1952.

Mwanzoni magari yalilazimika kukwea milima mirefu na kuzunguka eneo la Langalanga Nakuru na kwa jumla magari yalisindana umbali wa kilomita 5,160.

Makala ya kwanza pia yalikuwa na ufadhili wa pauni 1000 ,kutoka kwa kampuni mbili kila moja ikichangia pauni 500.

Joginder Singh alishinda makala ya mwaka 1965 ya Safari Rally akishirikiana na kakake Jaswant Singn wakiendesha aina ya Volvo PV44.

Pia walishinda mwaka wa 1974 na 76 wakitumia gari la Colt Lancer .

Shekhar Mehta wakishirikiana na Mike Doughty walishinda Safari Rally mara nne kati ya makala matano waliyoshiriki.

Mashindano yalibadilishwa jina na kuitwa
Kenya Safari Rally mwaka 1974, kufuatia kujiondoa kwa Tanzania kutokana misikosuko ya kiasisa.

Ian Duncan alikuwa Mkenya wa mwisho kushinda WRC Safari Rally mwaka 1994, akiendesha gari la Toyota Celica GT4 Turbo .

Mambo yalikuwa magumu maana hamana  dereva wa Kenya aliyemaliza mashindano katika makala ya mwisho ya WRC mwaka 2002.

Kutokana na maandalizi duni na kukosekana kudhibiti madereva mashindano ya Safari yaliondolewa katika kalenda ya WRC kabla ya kurejeshwa mwaka 2021.

Hata hivyo makala ya mwaka 2021 ya WRC yalikuwa tofauti ambapo madereva walishindana katika eneo la Naivasha pekee kinyume na awali ambapo mashindano yalikuwa mfumo wa kukimbia nyikani.

Sebastian Ogier aliibuka mshindi wa WRC Safari Rally mwaka 2021 akiendesha gari la Toyota Gazoo naye Kalle Rovanpera akatwaa ushindi mwaka 2022  pia kutoka kampuni ya magari ya Toyota Gazoo.

Makala ya mwaka 2023 yataandaliwa kati ya Juni 22 na 25  kurushwa mbashara na runinga ya KBC Channel 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here