Home Michezo Highway na Musingu zatinga fainali ya KSSSA

Highway na Musingu zatinga fainali ya KSSSA

0
kra

Shule za wavulana za Highway na Musingu kutoka eneo la Nairobi na Magharibi mtawalia, zimefuzu kwa fainali ya kesho ya mashindano ya kitaifa baina ya shule za upili yanayoendelea mjini Kisii.

Hatua hiyo inafuatia ushindi wa Highway wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Kirangari ya eneo la Kati wakati Musingu waliilaza St. Joseph (JOBO) ya eneo la Bonde la Ufa matuta tano kwa manne baada ya sare ya mabao mawili kwa mawili kwenye muda wa kawaida na wa ziada.

kra

kufuzu huko pia ni hakikisho la kushiriki michezo ya Afrika Mashariki baina ya shule za upili nchini Uganda.

Vile vile kutachezwa mechi ya kutafuta ntimu ya tatu baina ya Kirangari na JOBO na huenda ikashirikishwa miongoni mwa timu zitakazoelekea nchini Uganda.

Katika soka ya kina dada, shule ya wasichana ya Butere kutoka Magharibi na wenyeji Nyakach watachuana kwenye fainali baada ya Butere kuipiku Kombani ya eneo la Pwani mabao matatu kwa mawili nayo Nyakach ikaishinda St.Joseph bao moja kwa nunge.

Kesho pia kutachezwa finali ya voliboli ambapo Cheptil na Namwela zitakabana tena kwenye fainali baada ya kuchuana katika makundi ambapo Cheptil ilishinda seti tatu kwa mbili. Wakati huo huo, vidosho wa Kesogon watatifua kivumbi dhidi ya Kwanzanze.

Kwenye finali ya mchezo wa vikapu ya wachezaji watutu kila upande, St.Joseph ( Bonde la Ufa) imenyakua tuzo hiyo kwa kuwalemea wenyeji Onjiko kwa vikapu 16 kwa 14.

Zaidi ya hayo, vipusa wa St. Joseph wamenyakua taji la raga la wachezaji saba kila upande kwa alama 10-5 dhidi ya Kinale ya eneo la Kati.