Home Biashara Hazina ya Hustler yaongezewa shilingi bilioni 10

Hazina ya Hustler yaongezewa shilingi bilioni 10

0

Hazina kuu imependekeza kuongezwa  shilingi bilioni 10 kwa hazina ya Hustler, ambayo inatarajiwa kutoa mkopo wa riba nafuu kwa watu binafsi na biashara ndogo ndogo na zile za kadri.

Kulingana na Waziri wa Fedha profesa Njuguna Ndung’u, hazina hiyo iliyozinduliwa mwezi Novemba  mwaka jana, tayari imetoa mkopo wa shilingi bilioni 11, kati ya shilingi bilioni 20 ilizotengewa.

Hazina hiyo ambayo pia ni mpango wa kuwekeza, imeshuhudia uwekezaji wa shilingi bilioni 1.5 kutoka kwa wale wanaouchukua mikopo, huku shilingi zingine milioni 17 zikiwekezwa kwa hiari.

“Tumeshuhudia ukuaji mkubwa katika idadi ya kutuma na kupokea fedha kwa sasa ikiwa shilingi milioni 43.5. Idadi kubwa zaidi ya fedha zilizokopwa na mteja mmoja ni mara hamsimi zaidi,” alisema Waziri Prof. Ndung’u.

Wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Madaraka, serikali ilizindua awamu ya pili ya hazina ya hustler, inayolenga vyama vya ushirika na makundi, ambapo wanaweza pokea mkopo wa kati ya shilingi 20,000 na shilingi milioni moja.

Wanaokopa katika hazina hiyo wanatozwa riba ya asilimia nane kwa mwaka.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here