Home AFCON 2023 Hatujaamua tarehe ya AFCON 2025, asema Motsepe

Hatujaamua tarehe ya AFCON 2025, asema Motsepe

0

Kinara wa shirikisho la soka barani Afrika, Dkt. Patrice Motsepe amekiri kuwa kungali na utata kuhusu tarehe za kuandaliwa kwa fainali za kombe la AFCON mwaka 2025 nchini Morocco.

Akihutubu wakati wa kufungua mashindano ya AFCON nchini Ivory Coast Jumamosi usiku katika uwanja wa Alassane Ouattara, Motsepe alisema tarehe waliyopangia kundaa fainali hizo mwezi Juni na Julai inakinzana na fainali za kombe la dunia baina ya vilabu.

Motsepe aliongeza kuwa ipo haja ya kuandaa fainali za AFCON nyakati ambazo hazikinzani na kalenda ya soka ya ulaya ili iwe rahisi kwa wachezaji kuachiliwa kujiunga na timu za taifa.

Fainali za Kombe la Dunia kwa vilabu zitashirikisha timu 32 kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka ujao.

Website | + posts