Home Kaunti Hatua zachukuliwa kukabiliana na ajali za barabarani

Hatua zachukuliwa kukabiliana na ajali za barabarani

0

Halmashauri inayosimamia barabara nchini (KRB) imeanza ukaguzi wa maeneo yote hatari kwenye barabara ya ukanda wa kaskazini kufuatia ongezeko la ajali za barabarani.

Haya yalisemwa wakati halmashauri hiyo ilipotoa  msaada wa ambulensi na vifaa vya matibabu katika hosipitali ya Naivasha level IV katika juhudi za kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani kwenye  barabara kuu ya Nairobi- Nakuru.

Kwa mujibu wa Mhandisi Tom Omai, ambaye ni  mkurugenzi wa halmashauri hiyo, ongezeko la ajali humu nchini ni jambo la kusikitisha na hivyo basi kuna haja ya hatua za haraka kuchukuliwa.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa vya matibabu vilivyogharimu takriban shilingi milioni 16 kwa  wasimamizi wa hosipitali hiyo, Omai alisema ukaguzi wa muundo huo umeng’oa nanga kuanzia Mombasa hadi Malaba.

Kwa upande wake meneja wa hosipitali ya Naivasha Dkt. Bernard Warui alisema hosipitali hiyo uwahudumia takriban majeruhi 1,200 wa ajali kila mwaka.

Aidha aliongeza kuwa kulikuwa na haja ya kupanua kitengo cha wagojwa mahututi kwa haraka ambacho mwazoni kilikuwa na vitanda viwili ili kukabiliana na wahanga zaidi wa ajali za barabarani.

Huku watu takriban watu alfu nne wakipoteza maisha kila mwaka kufuatia ajali za barabarani, halmashauri hiyo imesema zoezi hilo linalenga kubuni njia za kudhibiti ajali za barabarani.

Website | + posts