Home Habari Kuu Hatua ya Uingereza kulifanyia kombora lake la Trident majaribio yagonga mwamba

Hatua ya Uingereza kulifanyia kombora lake la Trident majaribio yagonga mwamba

0
HMS Vanguard ni mojawapo ya nyambizi za nyuklia za Uingereza ambazo zinaweza kubeba silaha za nyuklia za taifa hilo.

Jaribio la kurusha kombora la Trident kutoka kwa nyambizi ya Royal Navy limegonga mwamba kwa mara ya pili mfululizo.

Jaribio la hivi punde zaidi lilifanywa kutoka katika nyambizi ya HMS Vanguard karibu na pwani ya mashariki ya Marekani.

Roketi za kuongeza nguvu za kombora hilo zilifeli na kutua baharini karibu na eneo la kurushia kombora hilo, kwa mujibu wa gazeti la Sun, ambalo liliripoti kwanza hitilafu hiyo.

Makombora matatu hubeba vichwa vya nyuklia vya Uingereza – silaha inayolazimika kutumika mwisho.

Hii ni aibu sana kwa Uingereza na Marekani ambayo ndio inayotengeneza kombora la Trident.

Majaribio ya Uingereza ya makombora ya Trident ni nadra, kwa sababu ya gharama. Bei ya kila kombora ni karibu £17m.

Waziri wa Ulinzi Grant Shapps na mkuu wa Jeshi la Wanamaji walikuwa kwenye meli ya HMS Vanguard wakati waliporusha kombora hilo lisilo na silaha katika pwani ya Mashariki ya Marekani mnamo Januari.

Lilipaswa kuruka maili elfu kadhaa kabla ya kutua bila madhara katika bahari ya Atlantiki kati ya Brazil na Afrika Magharibi. Badala yake kombora hilo lilidondoka ndani ya bahari karibu na liliporushwa.

Jaribio la awali kutoka kwa nyambizi ya Uingereza mnamo 2016 pia liliishia bila mafanikio, wakati kombora lilipotoka.

Wakati huo, gazeti la Sunday Times liliripoti kwamba kombora hilo aina ya Trident II D5 lilikusudiwa kurushwa maili 5,600 (kilomita 9,012) hadi eneo la bahari karibu na pwani ya magharibi mwa Afrika lakini lilielekea Marekani.

Chanzo cha kilichoharibika bado ni siri kuu, gazeti hilo liliripoti, lakini lilinukuu chanzo kikuu cha wanamaji kikisema kwamba kombora hilo lilipata hitilafu baada ya kurusha kutoka majini.

BBC
+ posts