Home Kimataifa Hatimaye chombo cha habari nchini Marekani chaeleza ukweli kuhusu Xinjiang

Hatimaye chombo cha habari nchini Marekani chaeleza ukweli kuhusu Xinjiang

0

Hivi karibuni, Shirika la Habari la CBS la nchini Marekani lilichapisha waraka kuhusu safari ya ujumbe wake mkoani Xinjiang.

Tofauti na habari zisizo za kweli zinazotangazwa na vyombo vingine vya habari vya nchi za Magharibi, waandishi wa habari wa CBS walieleza kile walichokiona na kukisikia walipokuwa mkoani humo.

Waandishi hao walitolea mfano kwamba, watu wa huko waliwaonyesha kila kitu na kwamba hawakuona ushahidi wa kile kinachoitwa “jela na vituo ambavyo watu wanashikiliwa.”

Badala yake, kile walichokishuhudia ni juhudi za wakazi wa huko kujenga reli za mwendo kasi, kujenga vituo vya umeme wa upepo, na kukuza utalii, na pia dansi za huko, uzalishaji wa mvinyo wa huko, na ukarabati wa vijiji.

Waandishi hao pia waliona kwamba, usimamizi na mazingira ya Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo wa Xinjiang, wakati wa usiku, yalikuwa ya utulivu.

Hata hivyo, kama chombo cha habari cha nchini Marekani, CBS ilijaribu kuweka uwiano, kwa kuongeza kauli zisizo za ukweli na kueleza kile wanachotaka, lakini ikilinganishwa na vyombo vingine vya habari vya nchini Marekani na nchi nyingine za Magharibi, ambavyo vinajulikana kwa kauli zao zisizo na ukweli kuhusu mkoa huo, CBS imepiga hatua moja karibu zaidi kueleza ukweli halisi wa Xinjiang.

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa, Xinjiang, ambayo imeondokana kwa mafanikio na janga la COVID-19, inaendelea kufunguka, na ukweli unagunduliwa na watu wengi zaidi wanaotoka nje ya China.

Uongo mkubwa ambao baadhi ya watu maarufu wa Marekani na nchi za Magharibi wamekuwa wakieneza kuhusu Xinjiang tayari unakabiliwa na mashaka na si wa kuaminika tena.

Ukweli ni kwamba, haijalishi ni kiasi gani CBS imejitahidi kuweka uwiano kuhusu ‘Xinjiang’ inayojengwa na Marekani na nchi za Magharibi, na Xinjiang ambayo wanahabari wake walijionea kwa macho yao, hiyo si njia pekee ya watu kutoka nje kujifunza ukweli kuhusu Xinjiang.

Katika mwaka mmoja uliopita, zaidi ya wageni 4,300 kutoka nje ya China na karibu makundi 400 kutoka nchi na mashirika ya kimataifa walialikwa kutembelea Xinjiang, wakiwemo maofisa wa serikali, mabalozi, viongozi wa kidini, wataalamu na wasomi, wanahabari na watu wa kawaida.

Watu hao walitembelea maeneo mbalimbali ya Xinjiang na kushuhudia wenyewe hali halisi, lakini jambo moja ambalo walikubaliana nalo ni kwamba ripoti mbaya kuhusu Xinjiang walizosoma katika vyombo vya habari vya nchi za Magharibi haziendani na kile walichokiona kwa macho yao na kukisikia kwa masikio yao.

Baadhi ya watu kutoka nchi za Magharibi daima wamekuwa wakipuuza ripoti zisizoendana na mawazo yao kuhusu Xinjiang kuwa ni propaganda ama zimetolewa baada ya wahusika kufadhiliwa na China.

Idadi kubwa ya watu hao hawajawahi kufika mkoani Xinjiang, na kwa wale wachache waliofika mkoani humo, wamefika wakiwa tayari na ajenda yao.

Lakini kadri muda unavyokwenda na utulivu na maendeleo ya Xinjiang vinazidi kukua, mafanikio nayo yanaonekana wazi. ‘Mfuko wa taarifa’ uliofumwa na watu wa Magharibi kwa hakika utapasuka! Katika siku za karibuni, ingawa Marekani na nchi za Magharibi zimeendelea kuzungumzia vibaya suala la Xinjiang, imekuwa ni mara chache ikilinganishwa na katika miaka michache iliyopita.

Sababu yake ni kwamba, watu wengi tayari wanaelewa kwamba, zile tuhuma kuhusu Xinjiang hazina ukweli wowote.Mkoa wa Xinjiang kwa sasa unaendeleza sekta yake ya utalii na inapokea wageni kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kutokana na mandhari yake ya kuvutia, tamaduni nzuri za huko, na rasilimali kubwa ya utalii, Xinjiang ni eneo ambalo lina ushawishi mkubwa kwa watalii.

Wale wanaoichafua Xinjiang wanajihusisha na vitendo ambavyo ni sawa na vya kigaidi, wakilenga kuharibu usalama, utulivu, na ustawi wa Xinjiang, jambo ambalo kamwe halitafanikiwa.

Carolin Nassoro
+ posts