Home Habari Kuu Harris ateua Tim Walz kuwa mgombea mwenza

Harris ateua Tim Walz kuwa mgombea mwenza

0
kra

Naibu Rais wa Marekani Kamala Harris ambaye pia anawania urais kupitia chama cha Democratic amemteua Gavana wa Minnesota Tim Walz kama mgombea mwenza kwenye uchaguzi wa mwezi Novemba.

Harris ametangaza hilo muda mfupi uliopita kupitia akaunti yake ya mtandao wa X lakini awali vyombo kadhaa vya habari vilikuwa vimetangaza.

kra

Kamala alipata uungwaji mkono kutoka kwa idadi inayohitajika ya wajumbe wa chama chake katika mkutano wa mtandaoni ulioandaliwa Ijumaa na hivyo kuwa mgombea rasmi wa urais.

Alipendekezwa na Rais Joe Biden ambaye alijiondoa kwenye kinyang’anyiro cha Urais Julai 21, 2024 kufuatia shinikizo kutoka kwa wanachama kadhaa baada ya kukosa kufanya vizuri kwenye mjadala na mwaniaji wa Republican Donald Trump.

Kamala Harris pia aliwasiliana na Walz kupitia video moja kwa moja ambapo alimjuza kwamba amemchagua yeye kama mgombea mwenza na wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kwanza wa kampeni pamoja huko Philadelphia.

Alitetea uteuzi wa walz kama mgombea mwenza akisema kwamba kujitolea kwake kupambania watu wa tabaka la chini ni mojawapo ya sifa zilizofanya ampendelee.

Mazingira aliyolelewa Walz na tasnia aliyochagua mapema maishani pia vinaimarisha alikofikia na Kamala anasema maisha yake yanakaribia kufanana na ya Walz.

Aliorodhesha pia mafanikio ya Gavana Walz katika jimbo la Minnesota hadi sasa kama vile kutetea haki ya kuavya mimba na likizo ya kulipwa ya familia na masuala ya kiafya.

Website | + posts