Timu ya taifa ya Soka Harambee Stars imeondoka Kampala mapema leo Jumamosi, kuelekea mjini Johanesburg, Afrika Kusini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2025.
Kenya imeratibiwa kumenyana na The Brave Warriors ya Namibia, siku ya Jumanne ijayo kaunzia saa moja usiku, kwa mechi ya pili ya kufuzu.
Stars iliambulia sare tasa katika mchuano wa kwanza uliosakatwa Ijumaa jioni katika uga wa Nelson Mandela jijini Kampala, Uganda.
Cameroon watawaalika Namibia katika mechi nyingine ya mzunguko wa kwanza katika kundi J leo Jumamosi usiku.