Home Michezo Harambee Stars yachapwa mabao 2-1 na Gabon

Harambee Stars yachapwa mabao 2-1 na Gabon

Harambee stars waliendelea kusuasua na kusababisha kufungwa bao la pili katika dakika ya 88 kupitia Guelor Kanga, huku mechi hiyo ikikamilika mabao mawili kwa bila.

0

Timu ya taifa ya soka harambee stars imeshindwa mabao mawili kwa moja na wenyeji Gabon, katika mechi ya kwanza ya kufuzu kwa fainali za Kombe la dunia mwaka 2026, iliyochezwa katika uwanja wa Franceville.

Vijana hao wa nyumbani walikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika ya 40 kupitia Masoud Juma, huku kipindi cha kwanza kikikamilika Stars wakiwa kifua mbele bao moja Kwa nunge.

Aidha katika kipindi cha pili Gabon walimakinika zaidi na kuimarisha mchezo wao dhidi ya stars, huku bidii yao ikizaa matunda mnamo dakika ya 60 ambapo walipata bao kupitia  Dennis Bouanga.

Harambee stars waliendelea kusuasua na kusababisha kufungwa bao la pili katika dakika ya 88 kupitia Guelor Kanga, huku mechi hiyo ikikamilika mabao mawili kwa bila.

Siku ya Jumatatu tarehe 20, Harambee stars watamenyana  na Ushelisheli Jijini Abidjan, Ivory Coast, nao Gabon waumize nyasi na Burundi siku ya Jumapili tarehe 19.

Kenya imeorodheshwa ya 110 huku Gabon ikiwa ya 86 katika msimamo wa FIFA.

Kundi F pia linajumuisha Ivory Coast, Ushelisheli, Burundi na Gambia huku viongozi wa kundi wakijikatia tiketi kwa dimba la Kombe la Dunia.