Timu ya taifa ya soka ya Kenya,Harambee Stars imendeleza mazoezi yake katika uwanja wa Nelson Mandela jijini Kampala Uganda, kujiandaa kwa mchuano wa kufuzu kwa kipute cha AFCON.
Harambee Stars iliwasili Kampala jana na inajiandaa kwa mechi ya kwanza ya kundi J, kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao dhidi ya Zimbabwe Ijumaa hii.
Kenya imelazimika kuchezea mchuano huo ugenini kutokana na ukosefu wa uwanja ulioidhinishwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Baadaye Harambee Stars wataelekea Afrika Kusini Jumamosi hii, kwa mechi ya pili dhidi ya Namibia Jumatatu ijayo.
Cameroon ndio wapinzani wengine wa Kenya katika kundi hilo.
Mechi ya kufuzu zinatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu, huku timu mbili bora kutoka kila kundi zikifuzu kwa kipute cha AFCON.
Fainali zijazo za AFCON zitaandaliwa baina ya Disemba mwak