Home Michezo Harambee Stars wapiga mazoezi ya mwisho kabla ya kukabiliana Ushelisheli

Harambee Stars wapiga mazoezi ya mwisho kabla ya kukabiliana Ushelisheli

0

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars imefanya mazoezi ya mwisho mjini Abidjan nchini Ivory Coast Jumapili kujiandaa kukabiliana na Ushelisheli Jumatatu usiku.

Kenya ni sharti washinde pambano hilo ili kufufua matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026, baada ya kuambulia kichapo cha magoli mawili kwa moja katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Gabon wiki iliyopita.

Harambee Stars ilisafiri kutoka mjini Franceville hadi Abidjan kujiandaa kwa mchuano huo.

Kocha Engin Firat ametoa tahadhari kwa wachezaji wake kutowapuuza wapinzani ambao walichakazwa mabao 9 kwa bila na Ivory Coast wiki iliyopita katika mchuano mwingine wa kundi F.

Ivory Coast, Gabon na Burundi wanaongoza kundi hilo kwa alama 3 kila moja.

Website | + posts