Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeendeleza mazoezi mjini Johannesburg Afrika Kuisni,kujiandaa kwa mechi ya pili ya kundi J, kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao nchini Morocco.
Kenya chini ya ukufunzi wa Engin Firat itakabiliana na wenyeji The brave Warriors ya Namibia, katika mchuano huo wa kesho jioni katika uwanja wa Orlando .
Stars waliotoka sare katika mechi ya kwanza dhidi ya Zimbabwe hawana budi kuishinda Namibia kesho ili kufufua matumaini ya kufuzu ,hususan baada ya Cameroon kuishinda Namibia mabao 2-0 katika pambano jingine.
Mchuano huo utapeperushwa mubashara kupitia runinga ya KBC Channel 1 kuanzia saa moja usiku.