Home Michezo Harambee Stars dhidi ya Urusi mechi ya kirafiki, kazi ipo!

Harambee Stars dhidi ya Urusi mechi ya kirafiki, kazi ipo!

0

Timu ya taifa ya kenya, Harambee Stars itapambana na Urusi katika mchuano kimataifa wa kujipiga msasa utakaosakatwa Jumatatu kuanzia saa moja usiku majira ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Titanic Sports Complex mjini Antalya, Uturuki.

Takriban wachezaji wote wako shwari kwa mtanange huo isipokuwa tu Ayub Timbe anayeuguza jeraha la mguu na beki Daniel Anyembe, ambaye hakuruhusiwa kuondoka na klabu yake.

Pambano hilo ni la mwisho la kujipima nguvu kwa Kenya kabla ya kucheza mchuano wa ufunguzi wa kundi F kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2016.

Kenya itafungua ratiba ya kundi F ugenini dhidi ya Gabon tarehe 13 mwezi ujao, kabla ya kuzuru Ushelisheli wiki moja baadaye kwa mchuano wa pili.

Harambee Stars itawaalika Burundi Juni 3 mwaka ujao na kuhitimisha mzunguko wa kwanza kwa kuwaalika Ivory Coast tarehe 10 mwezi Juni mwaka ujao.

Viongozi wa kila kundi watajikatia tiketi kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa mwaka 2026 na mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.

Website | + posts