Home Kimataifa Hamas yarusha roketi Tel Aviv

Hamas yarusha roketi Tel Aviv

0

Wanawake wawili wamejeruhiwa mjini Tel Aviv nchini Israel, baada ya wapiganaji wa Hamas kurusha msururu mpya wa roketi katika mji huo, kulingana na ripoti.

“King’ora kililia karibu saa mbili asubuhi mjini Tel Aviv. Kuna sehemu mbili ambazo (zilipigwa) na roketi,” shirika la habari la Reuters lilimnukuu mhudumu wa afya akisema.

“Mwanamke alijeruhiwa kwenye paja akiwa ndani ya gari lake.”

Hamas inasema mashambulizi ya hivi punde ni jibu la kuongezeka kwa vifo vya raia huko Gaza.

Jeshi la Israel linasema kuwa makombora 9,500, roketi na ndege zisizo na rubani zimerushwa dhidi ya Israel kutoka Gaza na maeneo mengine tangu tarehe 7 Oktoba.

Asilimia 12 ya makombora yaliyorushwa kutoka ndani ya Gaza yameanguka ndani ya ardhi ya Palestina, jeshi linasema.

Website | + posts
BBC
+ posts