Home Kaunti Halmashauri ya KPA yapongezwa kwa kuboresha kivukio cha Likoni

Halmashauri ya KPA yapongezwa kwa kuboresha kivukio cha Likoni

Kivukio cha Likoni kimerekodi idadi kubwa ya abiria wakati wa asubuhi na jioni.

0
Kivukio cha Feri cha Likoni, kaunti ya Mombasa.

Wakazi wa Mombasa wamepongeza halmashauri ya Usimamizi wa Bandari nchini (KPA) kwa kuboresha huduma za feri katika Kivukio cha Likoni tangu huduma za Shirika la Huduma za Feri nchini (KFS) ziunganishwe na zile za Halmashauri hiyo.

Kulingana na ripoti ya mkurugenzi mkuu wa KPA, Kapteni William Ruto, huduma za feri za saa 24 zinafanikisha zile za uchukuzi wa barabarani kwa kurahisisha usafiri watu milioni 126 na magari milioni 2.6 yanayovuka kivukio cha Likoni kila mwaka.

Wakazi wa Mombasa wamepongeza halmashauri ya bandari nchini (KPA), kwa kulainisha shughuli zake kwenye kivuko cha Likoni tangu huduma za feri ya kitaifa zilipounganishwa.

“Utoaji huduma bora unaendelea kuwa nguzo muhimu katika usafirishaji wa watu na bidhaa, na hivyo kuimarisha ukuaji wa uchumi wa kijamii hasaa katika sekta za kilimo, utalii, uzalishaji na sekta ya utoaji huduma,” alisema Ruto.

Kwa mujibu wa ripoti ya meneja mkurugenzi kapteni William Ruto, huduma hiyo ya feri inayohudumu saa 24 inatoa pongezi kwa uchukuzi wa barabarani kwa kuwezesha usafiri wa watu takriban milioni 126 pamoja na magari milioni 2.6 kwa mwaka kwenye kivuko hicho.

Kapteni Ruto aliongeza kuwa licha ya kufungwa kwa daraja la Liwatoni na pia kusitishwa kwa muda kwa huduma za feri ya Mtongwe, kivukio cha Likoni kimerekodi idadi kubwa ya abiria wakati wa asubuhi na jioni.

Kapteni Ruto alisema (KPA) imeanza mikakati ya kupunguza msongamano pamoja na kuziba mianya ya kupotea kwa mapato kwa kutumia mfumo wa malipo wa kiotomatiki, malango ya vizuizi ya kiotomatiki pamoja na barabara zenye alama mwafaka.

Aidha, usimamizi umefanya mageuzi ya taratibu za ukarabati wa kawaida kufanyika wakati idadi ya wateja iko chini pamoja na usiku ili kupunguza changamoto zinazoweza kuathiri wasafiri asubuhi na jioni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here