Vyuo vikuu vya umma vimekaa ngumu na kuwalazimisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo kulipia sehemu ya karo wanayohitajika kulipa, kabla ya kufanya mtihani wiki ijayo.
Hii inafuatia hatua ya serikali kuchelewa kutoa pesa za ufadhili wa masomo ya wanafunzi hao kwa wakati kama ilivyokuwa imeahidi.
Vyuo vikuu vimewaandikia wanafunzi wa mwaka wa kwanza arifa kuwaarifu wanahitajika kulipa sehemu ya karo kando na mkopo wa serikali kabla ya kufanya mitihani ya kufunga muhula kuanzia Disemba 6.
Wanafunzi waliruhusiwa kujiunga na vyuo hivyo mwezi septemba mwaka huu bila karo kufuatia agizo la Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu huku serikali ikiandaa mikopo na fedha za kugharimia masomo yao.