Home Kimataifa Hakimu wa Makadara Monica Kivuti amefariki

Hakimu wa Makadara Monica Kivuti amefariki

Akithibitisha kufariki kwa hakimu huyo, Jaji Mkuu Martha Koome, alisema Kivuti alifariki kutokana na majeraha ya risasi aliyopata.

0
Mahakama ya Makadara.
kra

Hakimu mwandamizi wa Mahakama ya Makadara aliyepigwa risasi na afisa wa polisi siku ya Alhamisi, ameaga dunia.

Akithibitisha kufariki kwa hakimu huyo, Jaji Mkuu Martha Koome, alisema Kivuti alifariki kutokana na majeraha ya risasi aliyopata.

kra

“Ni kwa huzuni kubwa nafahamisha taifa kuwa Mheshimiwa Monica Kivuti, hakimu mwandamizi katika mahakama za Makadara ameaga dunia kutokana na majeraha aliyopata aliposhambuliwa wakati wa kikao cha mahakama,” alisema Jaji Mkuu Martha Koome.

Aidha Jaji huyo Mkuu aliongeza kuwa.” Idara ya Mahakama inaomboleza na familia na marafiki wa hakimu huyo wakati huu mgumu wa majonzi,”.

Hakimu Kivuti alipigwa risasi kifuaniAlhamisi alasiri na mguuni na afisa wa polisi baada ya kutoa uamuzi kuhusu kesi iliyomhusisha mke wa afisa huyo wa polisi.