Home Kaunti Hakimu ahamishia hakimu mkuu kesi kwa kuhofia usalama wake

Hakimu ahamishia hakimu mkuu kesi kwa kuhofia usalama wake

0

Hakimu wa mahakama ya Port Victoria alijiondoa kwenye kesi ya ubakaji inayomkabili mwakilishi wa wadi ya Bunyala Magharibi Carlbenz Okonya kwa kile alichokitaja kuwa hofu juu ya usalama wake.

Badala yake alihamisha kesi hiyo hadi mahakama ya Busia kwa hakimu mkuu Edna Nyaloti.

Hakimu mkuu Nyaloti akizungumza mahakamani alielezea kwamba kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa katika mahakama ya Busia kwa sababu hakimu wa Port Victoria alihofia usalama wake.

Naye Nyaloti alisema kwamba iwapo atahisi kwamba yuko hatarini kwa sababu ya kesi hiyo, basi atalazimika kuomba maelekezo kutoka kwa jaji mkuu Martha Koome.

Mheshimiwa Okonya alishtakiwa mahakamani kwa kosa la kumbaka msichana wa umri wa miaka 14 mjini Busia Agosti 27 lakini akakanusha mashtaka mawili ya kubaka mwanafunzi na kujamiana na mtoto.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Faith Kaberia na Abraham Mumo ulipinga kuachiliwa kwa mshukiwa huyo kwa dhamana kwa kuhofia kwamba huenda akadhuru mashahidi.

Waliomba mahakama imzuilie mwakilishi huyo wa wadi kwa siku 14 lakini hakimu aliagiza azuiliwe kwa siku 9.

Website | + posts