Home Kimataifa Hafla ya kupandisha hadhi mji wa Eldoret yaahirishwa

Hafla ya kupandisha hadhi mji wa Eldoret yaahirishwa

0
kra

Hafla ya kupandisha hadhi mji wa Eldoret imeahirishwa kwa muda wa wiki moja kwa mujibu wa Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii.

Akizungumza na wanahabari leo asubuhi mjini Eldoret, Gavana Bii alifafanua kwamba hafla hiyo ambayo ingeandaliwa agosti 8, 2024, imeahirishwa hadi Agosti 15, 2024.

kra

Kulingana naye hatua ya kuahirisha hafla hiyo iliafikiwa baada ya mashauriano na serikali ya kitaifa.

Bii alisema pia kwamba maandalizi yote ya hafla hiyo yanayojumuisha usafishaji na unadhifishaji wa mji wa Eldoret yanaendelea vyema na muda ulioongezwa utafanikisha maandalizi hayo hata zaidi.

Rais William Ruto anatarajiwa kuongoza hafla ya utoaji wa cheti cha hadhi ya Jiji kwa Gavana Bii, hafla itakayoandaliwa katika eneo la Eldoret sports club.

Duru zinaarifu kwamba tarehe ya hafla hiyo imebadilishwa ili iwiane na wakati Rais Ruto atakuwa Eldoret kwa ajili ya tamasha ya washindi wa mashindano ya kitaifa ya muziki.

Mashindano hayo ya muziki kiwango cha kitaifa yanaendelea katika shule ya upili ya wasichana ya Moi mjini Eldoret.

Mashindano hayo ya siku 12 yamekutanisha wanafunzi wapatao elfu 130 na washirika wengine.

Website | + posts