Home Kimataifa Hafla ya kitaifa ya kuaga mwili wa Rais Hage Geingob kuandaliwa leo

Hafla ya kitaifa ya kuaga mwili wa Rais Hage Geingob kuandaliwa leo

0

Viongozi mbali mbali pamoja na wananchi wa taifa la Namibia wanakusanyika leo katika uwanja wa michezo wa Independence jijini Windhoek nchini Namibia kuuaga mwili wa marehemu Rais Hage Geingob.

Rais huyo wa Namibia Daktari Hage G. Geingob alifariki akiwa na umri wa miaka 82 Jumapili Februari 4, 2024 saa kumi alfajiri katika hospitali ya Lady Pohamba jijini Windhoek.

Hage Gottfried Geingob ni rais wa tatu wa taifa la Namibia na alianza kuhudumu katika wadhifa huo Machi 2015 hadi kifo chake hii leo.

Alihudumu kama waziri mkuu wa kwanza wa Namibia kati ya mwaka 1990 na 2002, na kati ya mwaka 2012 na 2015.

Alikuwa waziri wa biashara na viwanda mwaka 2008 hadi 2012 na amekuwa pia kiongozi wa chama tawala cha SWAPO tangu Novemba 2017 hadi leo.

Ameacha mke Monica Kalondo Geingos na watoto watatu.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni mmoja wa viongozi ambao wamewasili nchini Namibia kwa hafla ya leo, aliwasili jijini Windhoek jana jioni.

Website | + posts