Home Burudani H-art The Band kuzindua albamu mpya usiku wa manane leo

H-art The Band kuzindua albamu mpya usiku wa manane leo

0

Bendi ya wanachama watatu, Wachira Gatama, Kenneth Muya na Mordecai Mwini inayojulikana kama H_art The Band inapanga kuzindua albamu yao ya nne kwa jina “Time” usiku wa manane leo, mwanzo wa siku ya Ijumaa Oktoba 6, 2023.

Kwenye tangazo kupitia mitandao ya kijamii, bendi hiyo ilitangaza ujio wa kazi hiyo ya sanaa ambayo waliitaja kuwa zawadi kwa mashabiki wao na njia ya kusherehekea umbali wametoka.

Katika tangazo hilo, waimbaji hao walikumbuka jinsi walianza safari yao katika tasnia ya muziki kwa wimbo pendwa “Uliza Kiatu”.

Wanahadithia jinsi walizindua kibao hicho kwenye kituo kimoja cha redio na kushinda kwenye sehemu fulani za burudani wakitumai kukutana na watangazaji fulani wa redio ili wawapatie kazi hiyo yao ya kwanza.

“Siku ambazo tulikuwa tunacheza gitaa na kuimba kwenye barabara za Nairobi tukitumai kupata nauli ya kurejea nyumbani. Hatuamini jinsi muda umepita. Tangu wakati tuliishi pamoja kwenye nyumba ya chumba kimoja mtaani Kayole na sasa kila mmoja wetu anamiliki nyumba.” waliandika wanabendi hao.

Albamu hiyo ya “Time” wanasema imekuwa ikiandaliwa tangu Disemba 2022. Albamu za awali za bendi hiyo ni pamoja na “Made in The Streets”, “Simple man” na “Party Time”.

Kulingana na orodha ambayo imeshapishwa na Apple Music, Time ina nyimbo 11 ambazo ni, “Time”, “Habibty”, “Mada Dada”, “Kipenda Roho”, “W.Y.L.M”, “Umenikosea”, “Waenda”, “Barua”, “Karma”, “Mbio” na “Never Seen”.

Website | + posts