Home Michezo Gor wapigwa teke na CAF kushiriki mashindano ya ligi ya mabingwa

Gor wapigwa teke na CAF kushiriki mashindano ya ligi ya mabingwa

Hata hivyo haijabainika endapo Tusker FC waliomaliza katika nafasi ya pili watachukua nafasi hiyo ya Gor kuiwakilisha Kenya.

0

Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya, Gor Mahia wametimuliwa kushiriki masindano ya ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao na shirikisho la soka, CAF kwa ukiukaji wa sheria ambapo walikosa kuwalipa wachezaji watatu.

Kulingana na taarifa, wachezaji Jules Ulimwengu kutoka Burundi, Yangayay Sando Sando wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kipa wa Mali Adama Keita, waliishtaki Kogalo kwa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA ambapo usimamizi wa timu ulipewa hadi Julai 20, saa kumi na moja kuwalipa wanandinga ho la sivyo wafungiwe kushiriki ligi ya mabingwa msimu mpya.

Hata hivyo, haijabainika endapo Tusker FC waliomaliza katika nafasi ya pili watachukua nafasi hiyo ya Gor kuiwakilisha Kenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here