Gor Mahia wameibwaga AFC Leopards mabao mawili kwa bila katika derby ya Mashemeji ya 94 iliyosakatwa Jumamosi katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.
Gor Mahia almaarufu Sirkal, walichukua uongozi wa pambano hilo kunako dakika ya 22, Benson Omalla akidokolewa pasi murua na Austin Odhiambo na kukamilisha kipindi cha kwanza wakiwa kifua mbele.
Omalla alirejea kipindi cha pili na kutikisa nyavu kwa goli la pili huku Gor wakipata haki za kujitapa.
Katika mchuano mwingine wa Jumamosi, John Kiplagat alibusu nyavu mara mbili na kuwapa Murang’a Seal ushindi dhidi ya Sofapaka, Police FC wakailaza Nairobi City Stars bao moja kwa nunge huku Ulinzi Stars wakisajili ushindi wa kwanza msimu huu.