Klabu ya Gor Mahia iko jijini Cairo tayari kwa makabiliano dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, katika duru ya pili ya mchujo kuwania Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hiyo itasakatwa Jumamosi kuanzia saa moja usiku kesho katika uchanjaa wa Al Salam jijini Cairo.
Mabingwa mara 21 wa Kenya watakuwa na kazi ngumu kesho, baada ya kuambulia kipigo cha magoli matatu kwa bila, katika mkumbo wa kwanza uwanjani Nyayo.
Ili kufuuzu kwa hatua ya makundi Gor, wanahitaji ushindi wa mabao manne wa sifuri kesho dhidi ya wenyeji.