Home Michezo Gor Mahia wakaangwa tena, wafungiwa na FIFA kusajili wachezaji

Gor Mahia wakaangwa tena, wafungiwa na FIFA kusajili wachezaji

0

Mabingwa mara 20 wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia wamejipata kwenye njia panda kwa mara nyingine tena, baada ya kufungiwa kusajili wachezaji na FIFA.

Kwenye barua ya FIFA iliyotiwa sahihi na msimamizi wa maswala ya sheria Julien Deux, K’ogalo imepigwa marufuku kusajili wanandinga wapya baada ya kuchelewesha malipo ya mlinda lango wa Mali Adama Keita waliyekuwa wamemsajili.

FIFA imeamrisha FKF kuwafungia Gor Mahia kusajili wachezaji hadi watakapomlipa Keita.

Gor wamekuwa na masaibu kama hayo baada ya kupigwa marafuku kusajili wachezaji mwaka 2021 baada ya kushtakiwa na wachezaji Shafik Batambuze wa Uganda, Dickson Ambundo wa Tanzania na kocha Steven Polack.

Website | + posts