Home Michezo Gor Mahia kupambana na Al Merreikh

Gor Mahia kupambana na Al Merreikh

0
kra

Mabingwa wa Ligi Kuu Kenya,Gor Mahia watachuana na klabu ya Al Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini, katika mkumbo wa kwanza awamu ya mchujo kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mechi hiyo itapigwa Jumapili hii mjini Juba, huku marudio yakiandaliwa katika uchanjaa wa Nyayo Agosti 25.

kra

Gor chini ya ukufunzi wa kocha wa Brazil  Leonardo Neiva, wanarejea kwenye mashindano ya Ligi ya mabingwa mwaka huu, baada ya kutimuliwa mwaka uliopita kwa kukiuka sheria za usajii.

Hata hivyo Kogalo watazikosa huduma za mshambulizi wao tegemeo Benson Omala, aliyehamia klabu ya Alsafa SC inayoshirik ligi kuu nchini Lebanon.

Website | + posts