Mwimbaji wa nyimbo za injili Gloria Muliro ametangaza ujio wa tamasha lake la nyimbo za injili litakaloandaliwa jijini New York nchini Marekani.
Aliweka tangazo la tamasja hilo kwenye akaunti yake ya Instagram huku akihimiza mashabiki wake wanunue tiketi.
Tamasha hilo lililopatiwa jina la “Imanifest” litaandaliwa katika hoteli ya Noma jijini New York Septemba 14, 2024 kati ya saa kumi na moja jioni na saa nne usiku.
Kulingana na bango kwenye tovuti ya tamasha hilo, watakaokuwa jukwaani ni pamoja na Gloria, mume wake kwa jina Evans Sabwami, Angel Bernard na Timothy Kitui.
Tiketi zinauzwa dola 80 kwa watu wazima na dola 50 kwa watoto.
Gloria alihamia nchini Marekani baada ya kufunga ndoa na Sabwami nchini Kenya kisha wakafanya harusi nyingine nchini Marekani.
Awali alikuwa kwenye ndoa na mhubiri Eric Omba kabla ya kutalikiana.