Home Burudani Geoffery Kwatemba ateuliwa naibu mwenyekiti wa bodi ya KAMP

Geoffery Kwatemba ateuliwa naibu mwenyekiti wa bodi ya KAMP

0

Muungano wa watayarishaji muziki nchini Kenya yaani Kenya Association of Music Producers – KAMP umetangaza uteuzi wa aliyekuwa mtangazaji Geoffery Kwatemba kuwa naibu mwenyekiti wa bodi ya muungano huo.

Kulingana na tangazo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za KAMP, Kwatemba aliteuliwa kwa wadhifa huo kwenye mkutano wa bodi ulioandaliwa Alhamisi Juni 20, 2023.

Ujumbe huo ulielezea kwamba uteuzi huo ni sehemu ya mabadiliko yanayotekelezwa kwa lengo la kujumlisha mitazamo mipya na ujuzi katika muungano huo wa watayarishaji muziki.

Wadhifa huo ulikuwa ukishikiliwa na Rev. Anthony Kivuthi Musembi tangu Januari 12, 2023 chini ya uongozi wa mwenyekiti Bi. Angela Ndambuki na Bi. Faith Kithele.

Uongozi wa KAMP unamkaribisha Kwatemba ukinuia kushirikiana naye na kuhakikisha anakuwa na athari nzuri kama naibu mwenyekiti. Umeahidi kuendelea kupigania haki za watayarishaji muziki ili kuhakikisha ukuaji wa sekta ya muziki nchini.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Bi. Angela Ndambuki kurejeshwa kwenye wadhifa wa mwenyekiti wa bodi ya KAMP. Aliteuliwa kwa muhula mwingine kupitia mkutano uliofanyika Juni 22, 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here