Home Habari Kuu Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki alenga kufufua kilimo cha Kahawa

Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki alenga kufufua kilimo cha Kahawa

Muthomi alisema kuwa wataanda uchaguzi hivi karibuni kwenye shirika la Mwiru lililo na wanachama 1,450,

0
Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki.

Gavana wa kaunti ya Tharaka Nithi Muthomi Njuki, ameahidi kufufua kilimo na mashirika ya kahawa kwenye kaunti hiyo.

Kulingana na Gavana huyo, baadhi ya mashirika yameathiriwa kutokana na mizozo ya uongozi, na hivyo kusababisha kupungua kwa mapato na usambazaji wa kahawa.

Akizungumza afisini mwake mjini Chuka, Muthomi alisema kuwa wataanda uchaguzi hivi karibuni kwenye shirika la Mwiru lililo na wanachama 1,450, ambao watashiriki uchaguzi wa wanakamati wapya 10 watakao hakikisha utendakazi mwema wa viongozi.

Zaidi ya hayo, Gavana huyo ameonya kuwa sehemu za vileo zilizoko Mugwe, Kithangani na Magumoni lazima zithibitiwe ili kutoathiri mchakato wa uchaguzi.