Home Kimataifa Gavana wa Mombasa azindua kitengo cha kuhudumia watoto katika hospitali kuu ya...

Gavana wa Mombasa azindua kitengo cha kuhudumia watoto katika hospitali kuu ya Pwani

0
kra

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Nassir jana aliongoza uzinduzi wa kitengo cha kushughulikia watoto katika hospitali kuu ya eneo la Pwani almaarufu Coast General Hospital.

Nassir alisema kwamba hospitali za kaunti ya Mombasa zitakumbatia teknolojia katika utoaji huduma huku akifichua kwamba serikali ya kaunti inaunda mpango utakaowezesha wananchi kutoa maoni baada ya kupokea huduma.

kra

Alisema lengo kuu la mpango huo ambao utatekelezwa kwenye hospitali zote ni kuboresha utoaji huduma.

Kitengo hicho cha watoto cha ajali na dharura kina vifaa vilivyoongezwa kama vile wadi ya vitanda 14 na kinatarajiwa kuhudumia wagonjwa wapatao elfu 25, kila mwezi.

Kitengo hicho kimefanikishwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya kaunti ya Mombasa na wakfu wa benki ya Equity.

Gavana Abdullswamad alisema pia kwamba watoto wa umri wa chini ya miaka mitano hawatakuwa wakitozwa pesa zozote watakapokuwa wakipokea huduma katika hospitali zote za kaunti ya Mombasa.

Kulingana naye, hatua hiyo itawezesha watoto wa jamii maskini kupata huduma za matibabu lakini akasisitiza kwamba hatua hiyo itafaidi wakazi wa kaunti ya Mombasa pekee.

Alisema serikali ya kaunti tayari imetoa pesa kwa bima ya kitaifa ya matibabu NHIF ambazo zitagharamia huduma hizo kwa watoto.

Website | + posts