Home Habari Kuu Gavana wa Kwale azindua miradi ya ujenzi wa barabara

Gavana wa Kwale azindua miradi ya ujenzi wa barabara

Kulingana na Gavana Achani, miradi hiyo itaimarisha ukuaji wa uchumi na utangamano wa kijamii kwa wakazi wa kaunti hiyo.

0
Gavana wa Kwale Fatuma Achani azindua ujenzi wa barabara katika kaunti hiyo.

Gavana wa kaunti ya Kwale  Fatuma Achani, amezindua miradi ya ujenzi wa baarabara na uwekaji wa taa za barabarani, katika kaunti hiyo.

Kulingana na Gavana Achani, miradi hiyo itaimarisha ukuaji wa uchumi na utangamano wa kijamii kwa wakazi wa kaunti hiyo.

Alidokeza kuwa serikali yake itahakikisha inajenga barabara za ubora wa hali ya juu, zilizo na mabomba ya kupitisha maji taka na taa za barabarani.

Alielezea kujitolea kwake kushughulikia tatizo lililopo la ukosefu wa barabara, kupitia mpango kabambe wa ujenzi na ukarabati wa barabara.

Aidha Gavana huyo alisema wanakandarasi wanaojenga barabara hizo watafuatiliwa kwa karibu kuhakikisha barabara hizo ni za ubora wa hali ya juu, na zinakamilika kwa wakati ufaao.

Ili kuhakikisha kaunti ya Kwale inastawi, Achani alisema serikali yake itatekeleza miradi zaidi ya maendeleo ili kuwanufaisha wakazi na wawekezaji.

Website | + posts