Home Kimataifa Gavana Sakaja awateua wasimamizi wa hospitali za Level 5

Gavana Sakaja awateua wasimamizi wa hospitali za Level 5

0
kra

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amewateua wasimamizi wakuu wanne wa hospitali za Level 5 ili kuimarisha utoaji huduma wa vituo hivyo vya afya.

Walioteuliwa wanajumuisha Frederick Otieno Obwanda (Hospitali ya Mutuini), Alexander Irungu Wanjiru ( Hospitali ya Mbagathi), Christine Kiteshuo (Hospitali ya Pumwani) na Martin Alfred Wekesa Wafula (Hospitali ya Mama Lucy Kibaki).

kra

“Hospitali hizo ni taasisi ambazo zinapaswa kusimamiwa kitaalam. Kuanzia jinsi wagonjwa wananvyokaribishwa hadi katika vifaa vya hospitali, malazi, usambazaji wa dawa na chakula miongoni mwa mengine,” alisema Sakaja.

Gavana huyo pia alipanua mfumo wa usimamizi wa hospitali za Level 5 hadi Kwa hospitali zote za Level 4 katika kaunti hiyo.

Kulingana na Gavana huyo, uteuzi wa wasimamizi hao unalenga kuboresha utoaji huduma za matibabu kwa wakazi wa kaunti hiyo.

Website | + posts