Home Habari Kuu Gavana Nyong’o: Madaktari wanaogoma hawatalipwa

Gavana Nyong’o: Madaktari wanaogoma hawatalipwa

yong’o alidokeza kuwa ameagiza bodi ya utumishi wa umma ya kaunti hiyo kusimamisha mishahara ya madaktari hao, akisisitiza kuwa utawala wake hautalipia huduma ambazo hazijatolewa.

0
Gavana wa kaunti ya Kisumu Prof. Anyang' Nyong'o.

Gavana wa kaunti ya Kisumu Prof. Anyang Nyong’o, amesema kuwa madaktari wanaogoma wa kaunti hiyo, hawatapokea mshahara wa kipindi walichosusia kazi.

Akizungumza leo Alhamisi, Nyong’o alidokeza kuwa ameagiza bodi ya utumishi wa umma ya kaunti hiyo kusimamisha mishahara ya madaktari hao, akisisitiza kuwa utawala wake hautalipia huduma ambazo hazijatolewa.

“Kwa mujibu wa sheria za leba, serikali ya kaunti haitaoa malipo kwa kazi ambayo haijafanywa. Kwa hivyo, wahudumu wa afya ambao wamesusia kazi hawatalipwa kwa kipindi ambacho hawakufika kazini,” alisema Gavana huyo.

Ili kuhakikisha utoaji huduma za afya hautatizwi katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga, Nyong’o alisema serikali ya kaunti ya Kisumu iko katika harakati za kuwaajiri madaktari kwa mkataba wa muda mfupi, kutoa huduma muhimu.

Aidha Gavana huyo alilaani vikali mgomo huo wa madaktari, akisema kuwa serikali yake imekuwa ikijadiliana mara kwa mara na chama cha madaktari na wataalm wa meno KMPDU tawi la Nyanza, huku ikitekeleza mswala yao kwa utaratibu.

Website | + posts