Home Kaunti Gavana Nassir ahojiwa na polisi kuhusu kudhulumiwa kwa mwanablogu

Gavana Nassir ahojiwa na polisi kuhusu kudhulumiwa kwa mwanablogu

0
Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir, akihojiwa na wanahabari.
kra

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir, leo Alhamisi aliandikisha taarifa kwa afisi za maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, kuhusu kudhulumiwa kimapenzi na kutekwa nyara kwa mwanablogu mmoja wa kaunti hiyo.

Kiongozi huyo pamoja na mamake mzazi, walihusishwa katika kisa hicho.

kra

Baada ya kuandikisha taarifa, Gavana Nassir aliwaambia wanahabari kwamba, aliwahimiza maafisa hao wa DCI kuharakisha uchunguzi wao, huku akitoa wito kwa walio na habari zaidi kuhusu kisa hicho kuripoti kwa maafisa husika, kuhakikisha haki inapatikana kwa mwana blogu huyo.

Aidha Nassir alisema iwapo mamake mzazi atahitajika kuandikisha taarifa kwa maafisa hao wa DCI, yuko tayari kumpeleka.

“Nimesema hapo awali na leo nimefanya hivyo katika kituo cha polisi karibu nami. Nilifika katika afisi za DCIO na nimeandikisha taarifa. Jambo bora tunaloweza kufanya ni kwamba yeyote aliye na habari kuripoti kwa maafisa husika. Hiyo ndiyo njia ya pekee itakayohakikisha mwanablogu huyo anapata haki,” alisema Gavana Nassir.

“Hakuna binadamu yeyote aliye timamu anaweza sema tukio hilo ni sawa. Ninakashifu kisa hicho, na sasa tunapaswa kuzungumza kuhusu haki kupatikana kwa kijana huyo,” aliongeza Gavana huyo.

Washukiwa wanne tayari wameshtakiwa katika mahakama ya Shanzu mbele ya hakimu mkazi Robert Mbogo.

Wanne hao ni pamoja na Abdul Athman, Haji Babu, Esther Muthoni na Violet Adera, walikanusha mashtaka dhidi yao.

Wanazuiliwa katika gereza la Shimo La Tewa prison.

Website | + posts