Home Habari Kuu Gavana Mwangaza atafakari kuvunja bunge la Meru

Gavana Mwangaza atafakari kuvunja bunge la Meru

0
Naibu Gavana wa Meru Isaac Mutuma akiwa na Gavana Kawira Mwangaza
Naibu Gavana wa Meru Isaac Mutuma akiwa na Gavana Kawira Mwangaza

Gavana wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza amesema anatafakari kuvunja bunge la hiyo baada ya bunge hilo kuapa kulemaza shughuli zote za serikali ya kaunti.

Kawira amesimama kidete kuwa kamwe hatayumbishwa na vitisho vya wabunge wa kaunti hiyo kutishia kuwang’oa mamlakani mawaziri wake wanane .

Kulingana na katiba ya Kenya kipengee cha 192, Gavana anaweza kukuvunja bunge la kaunti kwa kumshauri Rais, iwapo kutatokea hali ya hatari itakayolemaza utendakazi.

Hata hivyo ni sharti aungwe mkono na asilimia 10 ya wapiga kura wote kabla ya Rais kuidhinisha pendekezo hilo.

Hali imekuwa tete katika bunge hilo kufuatia mfarakano kati ya gavana na waakilishi bunge wa kaunti hiyo ambao wamejaribu mara mbili bila mafanikio kumbandua afisini.