Home Habari Kuu Gavana Mung’aro aonya dhidi ya ujenzi haramu

Gavana Mung’aro aonya dhidi ya ujenzi haramu

0

Gavana wa Kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro ametoa ilani kuwa majengo yaliyojengwa katika Kaunti hiyo bila kibali rasmi kutoka serikali yake kuwa yatabomolewa.

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu, Mung’aro aliwashutumu maafisa wa kitengo cha upelelezi Jinai (DCI) kwa kushirikiana na wanyakuzi wa ardhi kuwanyanyasa wakazi wa Kaunti hiyo.

“Malalamishi kuhusu vitisho kutoka kwa watu kutoka kwa DCI, sitaki kuyasikia, tuna sheria za Kaunti, na tuna sheria zetu ndogo,” alisema Mung’aro.

“Ukijenga bila kibali, tutaangusha majengo, ukijenga ukuta au nyumba ya ghorofa tutaiangusha.”

Mung’aro alisema kuwa ni kaunti pekee iliyo na vibali vya ujenzi ni jukumu la kaunti na ilani yoyote ya kutimuliwa au idhini ya ubomoaji lazima itoke kwa ofisi zinazofaa.

Gavana Mung’aro alitishia kukabiliana na maafisa wa DCI, ambao baadhi yao wameshitakiwa kwa kuingilia kesi za ardhi zisizo kwenye mamlaka yao.

Kauli ya gavana huyo inajiri siku chache baada ya wakazi kutoa madai kupokea barua za kufurushwa zinazodaiwa kuandikwa na matajiri wenye uhusiano wa karibu na kwa ushirikiano na maafisa wafisadi serikalini.

Alphas Lagat
+ posts